Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:16

Viongozi wa NAM waisihi Israel kusitisha vita Gaza mara moja


Viongozi wa nchi wajumbe wa NAM wakiwa katika picha ya pamoja huko Kampala Uganda Januari 19, 2024. Picha na REUTERS/Abubaker Lubowa
Viongozi wa nchi wajumbe wa NAM wakiwa katika picha ya pamoja huko Kampala Uganda Januari 19, 2024. Picha na REUTERS/Abubaker Lubowa

Viongozi wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) siku ya Ijumaa wamelaani kampeni ya kijeshi ya Israel huko Gaza na kutaka usitishaji wa mapigano hayo mara moja, wakati wa mkutano wa kila mwaka wa wajumbe 120 wa jumuiya hiyo.

Dazerni ya wakuu wa nchi na maafisa waandamizi kutoka NAM, iliyoundwa rasmi mwaka 1961 na nchi zilizopinga kujiunga na upande wowote wa kambi kuu mbili wakati wa enzi ya vita baridi wanahudhuria mkutano unaofanyika kampala, Uganda.

Israel ilianzisha mashambulizi yake huko Gaza baada ya shambulio la kundi la kiislamu la Hamas la Oktoba 7 ambalo maafisa wa Israel wanasema lilisababisha vifo vya zaidi ya Waisrael 1,200 na raia wa kigeni na watu 240 kuchukuliwa mateka.

Kampeni hiyo ya kijeshi imeua zaidi ya Wapelestina 24,000, kulingana na mamlaka ya afya ya Gaza.

“Tangu Oktoka 7 tumeshuhudia moja ya matendo ya kikatili ya mauaji ya kimbari ambayo hayajawahi kurekodiwa katika historia,” Makamu wa rais wa Cuba Salvador Valdes Mesa alisema alipokuwa akiwahutubia wajumbe.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ametoa wito wa kusitisha mara moja kwa kile alichokiita “vita visiyo vya haki dhidi wa wananchi wa Palestina”.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG