Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:24

Serikali ya Benin yataka kurejesha uhusiano na utawala wa kijeshi wa Niger


Rais Patrice Talon akipeana mkono na jaji baada ya kuapishwa kuwa rais Benin huko Cotonou, Benin, April 6 2016. Picha na Reuters
Rais Patrice Talon akipeana mkono na jaji baada ya kuapishwa kuwa rais Benin huko Cotonou, Benin, April 6 2016. Picha na Reuters

Rais wa Benin Patrice Talon siku ya Alhamisi amesema anataka kurejesha uhusiano kati ya nchi yake na nchi jirani ya Niger, ambayo hivi sasa inatawaliwa na viongozi wa kijeshi.

Katika hotuba yake kwa taifa ya mwisho wa mwaka aliyoitoa katika bunge, Talon alieleza “anataka kuona uhusiano wa haraka unaimarishwa kati ya Benin na nchi zilizopinduliwa.”

Amesema hajashindwa “kuzungumzia kwa busara na kwa kurudia, ujumbe kwa mataifa haya ndugu, hususan Niger” ambako rais Mohamad Bazoum aliondolewa madarakani mwezi Julai.

Kuna “wakati wa kulaani, kuna wakati wa kudai na kuna wakati wa kutathmini na kuzingatia”

Washirika wetu wafanye jukumu lao na waseme wazi nia yao ni nini, na wanataka kitu gani kutoka Jumuiya ya kimataifa,” aliwaambia wabunge.

Vikwazo kwa Niger viliwekwa na kanda ya Afrika Magharibi ECOWAS, vimesababisha kufungwa mpaka wa Niger na Benin na kuathiri vibaya uchumi.

Benin imeona mapato yakipungua baada ya usafirishaji wa bidhaa kwenda Niger kupitia bandari zake kusitishwa.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) iliiwekea Niger vikwazo vikubwa vya kiuchumi na vya kifedha pamoja na kusitisha biashara baada ya mapinduzi ya Julai 26.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG