Afrika Kusini ilifungua kesi ya dharura katika mahakama ya ICJ ikisema kwamba Israel inakwenda kinyume na Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa Umoja wa Mataifa, uliotiwa saini mwaka 1948 kufuatia mauaji ya Holocaust, na inataka mahakama hiyo kusimamisha mara moja operesheni zake za kijeshi huko Gaza ambazo zilianzishwa baada ya mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7.
Namibia, nchi ya kusini mwa Afrika ambako mauaji ya halaiki ya kwanza ya karne ya 20 yalifanyika chini ya utawala wa kikoloni wa Ujerumani, inapinga uungaji mkono wa Ujerumani wa dhamira ya mauaji ya kimbari ya taifa la kibaguzi la Israel, ofisi ya rais ilisema katika taarifa yake Jumamosi jioni.
Akilalamikia kushindwa kwa Ujerumani kupata somo kutokana na historia yake ya kutisha, Rais wa Namibia Hage Gein-gob alionyesha wasiwasi mkubwa kwa uamuzi wa serikali ya Ujerumani Ijumaa wa ku[inga mashtaka ya uadilifu yaliyowasilishwa na Afrika Kusini.
Forum