Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:07

Mahakama ya Kimataifa ya Haki yaanza kusikiliza kesi iliowasilishwa na Afrika Kusini, dhidi ya Israel


Watu wakiwa ndani ua ukumbi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini The Hague, wakisikiliza kesi iliowasilishwa na Afrika Kusini, dhidi ya Isarel.
Watu wakiwa ndani ua ukumbi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini The Hague, wakisikiliza kesi iliowasilishwa na Afrika Kusini, dhidi ya Isarel.

Majaji kwenye mahakama ya Kimataifa ya Haki Alhamisi wameanza siku mbili za kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini, ikiishutumu  Israel kwa kutekeleza mauaji ya kimbari katika vita vyake huko Gaza.

Afrika Kusini imeiomba mahakama hiyo iamuru kusitishwa mara moja kwa kampeni ya Israel huko Gaza, ambako Israel imesema kwamba nia yake ni kuliangamiza kundi la Hamas, kufuatia shambulizi la Oktoba 7 kusini mwa Israel.

Waraka uliowasilishwa na Afrika Kusini unasema kwamba ungependa kuona mahakama hiyo ikiiwajibisha Israel kwa kukikuka mkataba unaopinga mauaji ya halaiki, pamoja na kuhakikisha uwezekano wa ulinzi kamili wa wapalestina waliopo Gaza, ambao wako kwenye hatari kubwa na ya haraka kutokana na kuendelea kwa vitendo vya mauaji ya kimbari.

Israel imezipuuza tuhuma hizo kuwa hazina msingi. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Jumatano jioni alisema kwamba vikosi vya Israel vinafanya kila viwezalo kuzuia vifo vya raia, wakati akiwashutumu wanamgambo wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao.

“Israel inapambana na magaidi wa Hamas, na wala siyo raia wa Palsetina, na tunafanya hivyo kwa kuzingatia sheria zote za kimataifa,” amesema Netanyahu.

Forum

XS
SM
MD
LG