Taifa la Isreal ambalo lilibuniwa baada ya mauaji ya wayahudi, limekanusha vikali shutuma zilizofikishwa kwenye mahakama hiyo na Afrika Kusini, ikiwa moja ya kesi kubwa zaidi kuwahi kufikishwa katika mahakama ya kimataifa, na kuvutia mtizamo wa kimataifa na waandamanji kutoka mirengo yote, nje ya jengo la mahakama hiyo.
Mawakili wa Afrika Kusini Alhamisi wameomba mahakama hiyo Alhamisi kuiamuru Israel isitishe mara moja operesheni zake za kijeshi katika eneo lililozingirwa la pwani ambalo ni makazi ya takriban wapalestina milioni 2.3. Uamuzi wa ombi hilo huenda ukachukua wiki kadhaa, ingawa kesi huenda itachukua miaka kukamilika.
Forum