Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 06:05

Shinikizo laongezeka kwa jeshi la polisi Hong Kong kuwajibika


Polisi wa kuzuia ghasia wakimshikilia mmoja wa waandamanaji wakati wakiwatawanya walipokuwa wakipinga sheria mpya ya usalama wa taifa mjini Hong Kong on Julai 1, 2020, katika maadhimisho ya miaka 23 ya Hong Kong kukabidhiwa China kutoka utawala wa Uingereza.
Polisi wa kuzuia ghasia wakimshikilia mmoja wa waandamanaji wakati wakiwatawanya walipokuwa wakipinga sheria mpya ya usalama wa taifa mjini Hong Kong on Julai 1, 2020, katika maadhimisho ya miaka 23 ya Hong Kong kukabidhiwa China kutoka utawala wa Uingereza.

Uamuzi wa Mahakama moja Hong Kong umeimarisha matakwa ya kuwepo mfumo huru wa kupokea malalamiko dhidi ya polisi wakati kunaongezeko la kilio ndani na nje ya nchi juu ya madai ya kukamatwa watu kiholela na polisi kutumia nguvu kupita kiasi. 

Kuna wakati ilikuwa inachukuliwa ni mji mzuri katika bara la Asia, jiji lenye jeshi la polisi 30,000 imara linakabiliwa na shutuma kwa vitendo vyake wakati wa maandamano yaliyoenea kote dhidi ya serikali iliyoikumba Hong Kong mwaka 2019.

Mabomu ya machozi, maji yenye nguvu, gesi za pilipili na virungu vilitumiwa kwa kiasi kikubwa na polisi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa hawajakata tamaa..

Mwezi Novemba 29, Mahakama ya Mwanzo ilitoa uamuzi unaosaidia hoja ya chama cha Waandishi wa Habari Hong Kong, ikisema mfumo uliokuwepo hautoshelezi katika kuchunguza malalamiko dhidi ya polisi wanaovunja sheria ya haki za binadamu za jiji hilo juu ya vitendo vya utesaji na ukatili.

Pia kushindwa kwa jeshi la polisi kuwataka maafisa wa kutuliza ghasia kuweka wazi namba zao kwa kuvaa beji wakati wa maandamano ikiwa ni kuvunja sheria ya haki za kiraia na kisiasa, mahakama hiyo imesema.

“Iwapo serikali bado inaiheshimu mahakama, iwajibike kurekebisha tatizo hilo,” Eric Cheung Tat-ming, amesema mhadhiri mkuu na mkurugenzi wa kituo cha kutoa elimu ya sheria katika chuo kikuu cha Hong Kong

Iwapo serikali itashindwa katika rufaa yake [Mahakama ya Rufaa], itahitaji kuchukua muda kidogo kuanzisha mfumo mpya. Iwapo maafisa wa serikali watapuuza mapendekezo ya jaji, itachukuliwa kuwa inakiuka uamuzi huo,” amesema.

Cheung anasisitiza matakwa ya kupatikana taasisi ya kujitegemea kushugulikia malalamiko na kuchukua hatua za nidhamu na tuhuma zozote za uongo dhidi ya maafisa wa polisi. Wanaounga mkono mfumo huo ni pamoja na wabunge wanaosimamia demokrasia.

Ameongeza kuwa serikali italazimika kutafuta utaratibu wa kutatua mambo makuu mawili aliyoeleza jaji katika uamuzi wake – kutokuwepo usimamizi huria katika mfumo uliokuwepo wa kupokea malalamiko dhidi ya polisi na polisi kutovaa beji zao kuwatambulisha.

C.M Chan, wakili na mkuu wa kituo cha Utawala wa Sheria cha Chuo cha Utafiti wa Sera Hong Kong, taasisi inayojitegemea, amependekeza kuwa serikali ya Hong Kong kitu kinachofanana na Tume ya Malalamiko Huru ya Polisi Uingereza, ambayo anaifananisha kama “chui mwenye meno” ambacho kina mamlaka ya kuanzisha uchunguzi.

Katika mtizamo wa utawala mzuri wa sheria, serikali ni lazima isikilize mapendekezo ya mahakama,” amesema, akiongeza kuwa, “ Hivi sasa, unapolalamika dhidi ya polisi na malalamiko hayo yanakwenda polisi na IPCC inafuatilia tu uchunguzi huo,” amesema, akikusudia Baraza la Malalamiko Huria la Polisi Hong Kong.

XS
SM
MD
LG