Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:34

Seneta Menendez atarajiwa kufika mahakamani huko New Jersey kujibu mashtaka ya kusukuma maslahi ya Wamisri kwa siri


Seneta Bob Menendez (D-NJ)
Seneta Bob Menendez (D-NJ)

Seneta wa New Jersey Bob Menendez anatarajiwa kufika mahakamani leo huko New York kujibu mashtaka ya serikali kuu yanayomshutumu mdemocrat huyo kwa kutumia wadhifa wake wenye nguvu kusukuma kwa siri maslahi ya Wamisri.

Mashtaka hayo yamedai kwamba Menendez alifanya upendeleo kwa wafanyabiashara wa New Jersey badala ya malipo ya pesa taslimu na dhahabu.

Menendez atatokea kwa mara ya kwanza katika mahakama ya Manhattan kufuatia wito uliozidi kuongezeka kutoka kwa wafanyakazi wenzake ikiwemo wengine kutoka chama chake kwamba ajiuzulu.

Kesi yake inakuja siku moja baada ya mwanamme mmoja kushtakiwa kwa njama ya kumhonga Menendez na kufikishwa katika mahakama ya serikali kuu huko New York.

Wael Hana amekana mashtaka yake ikiwemo njama ya kufanya vitendo vya rushwa.

Hanna alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Kennedy huko New York jumanne baada ya kurejea kwa hiari kutoka Misri kukabiliana na mashitaka na kuachiliwa huru akisubiri kesi, aliamriwa kulipa dhamana ya dola laki tatu fedha taslimu na bondi ya dola milioni tano.

Forum

XS
SM
MD
LG