Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:54

Biden awa rais wa kwanza kushiriki mgomo wa wafanyakazi Marekani


Joe Biden, Jumanne amekuwa rais wa kwanza wa Marekani, aliyepo madarakani kushiriki kwenye  mgomo wa wafanyakazi wakati alipojiunga na wafanyakazi katika viunga vya jiji la Detroit.

Maandamano yanaingia wiki ya pili ya mgomo wao wakitaka malipo zaidi, muda mfupi wa kufanyakazi na mahitaji mengine kutoka viwanda vikubwa vitatu vya kutengeneza magari.

Wafanyakazi wanataka nyongeza ya malipo kwa asilimia 40, kufanyakazi kwa saa 32 kwa wiki na zaidi wakigusia namna kampuni zinavyo pata faida.

Rais Biden amekuwa mwangalifu wa kutosema hadharani ni madai gani kati ya yale wanayoyahitaji anayaunga mkono ama kwa kiwango gani anaunga mkono maandamano ya wafanyakazi hao.

Forum

XS
SM
MD
LG