Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:10

Wabunge kujadili kufungwa au kutofungwa kwa serikali ya Marekani


Rais Biden baada ya kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Marekani huko Washington Machi 1, 2022. Picha na Julia Nikhinson / POOL / AFP.
Rais Biden baada ya kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Marekani huko Washington Machi 1, 2022. Picha na Julia Nikhinson / POOL / AFP.

Bunge la wawakilishi na seneti Marekani limepanga kuchukua njia tofauti katika vita juu ya matumizi ya serikali wakati zimesalia siku tano hadi tarehe ya mwisho ambayo inaweza kulazimisha maeneo mengi ya serikali kufungwa kwa mara ya nne katika muongo mmoja.

Seneti inayodhibitiwa na wa- democrat inapanga kupiga kura juu ya mswada wa ufadhili wa kusimamishwa uungawaji mkono wa msaada wa pande mbili ambao utapelekea serikali kuendelea kufanya kazi baada ya fedha zake kuisha usiku wa manane wa siku ya jumamosi, hatua itakayotoa nafasi kujadiliana zaidi kuhusu matumizi ya mwaka mzima.

Wakati huohuo spika wa baraza la wawakilishi wa chama cha Republican Kevin McCathy amelenga kusitisha uasi wa wanachama wenye msimamo mkali wa baraza lake mwenyewe akitaka kusukuma mbele miswada minne ya matumisi ya mwaka mzima ambayo inaangazia vipaumbele vya kikonsevativu na kutokuwa na nafasi ya kuwa sheria.

Bunge limeshawahi kufunga serikali mara 14 tangu mwaka 1981 ingawa pengo la fedha za matumizi ya serikali zilidumu kwa siku moja au mbili, na hatua hiyo haijawahi kuwa na matokeo yoyote makubwa katika uchumi wa dunia.

Forum

XS
SM
MD
LG