Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:09

Biden asema anashughulikia mambo yenye umuhimu kwa Wamarekani na siyo uwanja wa siasa


Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden anasema “amelenga katika mambo ambayo Wamarekani wanayataka” na siyo uwanja wa siasa.

Hii ni kufuatia wabunge katika Baraza la Wawakilishi wiki iliyopita kufungua hoja ya shutuma za kutaka kumshtaki rais kumuondoa madarakani kuwa alinufaika na makubaliano ya kibiashara ya mtoto wake Hunter.

Wademocrat wameiita hatua hiyo ni ya ovyo. Yote haya yamekuja wakati wabunge lazima wafikie makubaliano na Biden kuhakikisha serikali haifungwi baada ya Septemba 30 tarehe ya mwisho ya kufadhali matumizi ya serikali kuu.

Rais wa Marekani Joe Biden alionekana kanisani katika jimbo analotoka la Delaware, siku chache baada ya Warepublican katika Baraza la Wawakilishi kufungua kesi ya kutaka kumuondoa madarakani, wakielezea shutuma za mwenendo wa rushwa. White House inaiita ni ujinga wa kisiasa.

Wiki hii iliyopita, Spika wa Bunge Kevin McCarthy aliongea na vyombo vya habari nje ya ofisi yake katika jengo la bunge. “Wabunge Warepublican wamegundua shutuma nzito na za uhakika kuhusiana na mwenendo wa Rais Biden. Zikichukuliwa pamoja, hizi shutuma zinatoa picha ya utamaduni wa rushwa.”

McCarthy aliendelea kuelezea hizo shutuma kama ni ‘matumizi mabaya ya madaraka, kuingilia sheria na rushwa ambapo inahitajika uchunguzi zaidi kufanywa na Baraza la Wawakilishi.’Wademocrat wanasema hizi ni siasa za vyama katika wakati mbaya sana.

Kiongozi wa Walio Wachache Hakeem Jeffries, Mdemocrat anasema, “White House itaendelea kushirikiana, kwa sababu hakuna cha kuficha. Hakuna ukweli katika rekodi unaopendekeza kwamba Rais Biden amejihusisha katika kufanya makosa ambayo yanapelekea kushtakiwa kuondolewa madarakani. Hakuna ukweli katika rekodi unaopendekeza kwamba Rais Biden alivunja sheria kwa hali yoyote ile. Hii hoja ya kutaka kumsthaki kumuondoa madarakani ni kinyume cha sheria.”

Warepublican wanasema wanataka habari zaidi zinazohusisana na shutuma hizo.

Mbunge Nancy Mace, Mrepublican anasema, “ukweli uko kila mahali. Kuna ujumbe wa maandishi. Kuna barua pepe. Kuna mashahidi. Kuna watoa habari. Kuna mikutano. Kuna simu zilizopigwa. Kuna chakula cha jioni, na huwezi kusema huu ni moshi mdogo tun a hatutaufuata moto.”

Rais wa zamani Donald Trump,mgombea wa sasa wa mbele Mrepublican anayewania urais, amejikuta akikabiliwa na zaidi ya makosa 40 ya uhalifu katika mahakama mbali mbali, anasema anaunga mkono serikali kufungwa kama Baraza la Wawakilishi ambalo lina Warepublican wengi hawapati kile alichokiita ‘makubaliano mazuri’ kwa matumizi ya muda mfupi. Maelezo ya ‘makubaliano ya haki’ bado hayako bayana.

Mustakbali wa Biden na McCarthy umefungamana katika hoja hii ya kutaka kumshtaki rais kumuondoa madarakani. Baada ya kutoa hoja moja, baraza kamili litapiga kura iwapo rais ni vyema ashtakiwe , na kuchochea kesi katika Baraza la Senate kama kura itakuwa ya ndiyo.

Wakati huo huo, Bunge lina siku kadhaa za kupitisha kuendelea kwa matumizi kwa muda mfupi au serikali ifungwe.

Baadhi warepublican waconservative wanataka matumizi yakatwe zaidi kuliko kile ambacho Spika McCarthy amekubali katika makubaliano ya bajeti na Biden mapema mwaka huu.

Habari hii imeandikwa na mwandishi wa VOA Arash Arabasadi.

Forum

XS
SM
MD
LG