Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:18

Hunter Biden afunguliwa mashitaka ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria


Mwana wa kiume wa Rais wa Marekani Joe Biden, aliyefunguliwa mashitaka Alhamisi.
Mwana wa kiume wa Rais wa Marekani Joe Biden, aliyefunguliwa mashitaka Alhamisi.

Hunter Biden mwana wa kiume wa Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi amefunguliwa mashitaka na viongozi wa mashitaka, akituhumiwa kununua bunduki katika muda aliokiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine, wakati akidanganya kuwa hakuwa akitumia, ili aweze kuuziwa.

Mashitaka hayo dhidi ya Hunter mwenye umri wa miaka 53 mara moja yamezua mjadala mpya kwenye kampeni za rais wa Marekani mwaka ujao. Baba yake Joe Biden anapanga kuwania tena urais wakati mpinzani wake mkuu wa Repablikan, Donald Trump akikabiliwa na mashitaka manne ya jinai, yenye jumla ya kesi 91 za kusikilizwa.

Mashitaka dhidi ya Hunter Biden hayakuwa yakitarajiwa, kwa kuwa mwongoza mashitaka maalum David Weiss siku chache zilizopita alisema kwamba yangewasilishwa mwishoni mwa mwezi. Wakili wa Hunter, Abbe Lowell amekashifu Weiss kwamba ameshinikizwa kisiasa na Warepablikan katika kumfungulia mashitaka.

Forum

XS
SM
MD
LG