Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:37

Wamarekani wakusanyika kote nchini kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 ya mashambulizi ya kigaidi

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na Gavana wa New York Kathy Hochul wakihudhuria kumbukumbu ya 22 ya shambulizi la kigaidi katika eneo lililokuwa ni kituo cha biashara cha Kimataifa , New York, September 11, 2023.

Bendera nyingi za Marekani zilipeperushwa Pentagon Jumatatu asubuhi na Wamarekani wamekusanyika kote nchini  kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 ya mashambulizi ya kigaidi ya septemba 11.

Rais wa Marekani Joe Biden anarejea Washington, DC, kutoka katika zira yake ya nje ya nchi huko India na Vietnam.

Rais wa Marekani Joe Biden REUTERS/Evelyn Hockstein
Rais wa Marekani Joe Biden REUTERS/Evelyn Hockstein

Rais atazungumza katika maadhimisho kwenye kambi ya jeshi ya Elmendorf –Richardson huko Anchorage, Alaska.

Wakati huo huo Makamu wa Rais Kamala Harris ni miongoni mwa maafisa waliochaguliwa ambao watahudhuria katika matukio ya kumbukumbu ya septembea 11 Mjini New York.

Jumuiya kote nchini zinatoa heshima zao zikikaa kimya , kugonga kengele , kuwasha mishumaa na shughuli nyingine.

Habari hii inatokana na vyanzo vya habari mbalimbali.

Forum

XS
SM
MD
LG