Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:58

Wamarekani waadhimisha miaka 21 tangu mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11


Kijana aweka bendera wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 21 tangu mashambulizi ya Septemba 11, 2001.
Kijana aweka bendera wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 21 tangu mashambulizi ya Septemba 11, 2001.

Wamarekani wameadhimisha miaka 21 tangu mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, ambapo rais Joe Biden alitliembelea jengo la Pentagon, Makamu Rais Kamala Harris aliungana na waombolezaji mjini New York na mke wa rais Jill, alikuwa Pennsylvania, ili kuwakumbuka watu 3,000 walofariki siku hiyo.

Rais Biden aliweka shada la maua nje ya jengo ambalo ndege nambari 93 ilianguka huku mvua ikinyesha. Akiwahutubia waliohudhuria sherehe hizo, alitaja na kukumbusha jinsi wamarekani walivyoungana kujibu mashambulio hayo na kuapa kwamba “kamwe hawatawaacha” kuendelea kupigana dhidi ya vitisho vya ugaidi.

Biden alisema kwamba ana matumaini wamarekani hawatasahau kwamba wakati wa siku hizo za giza waliungana. Na kujali hali ya kila mtu. Waliungana, na hivyo anatoa wito kwa wamarekani kuungana pamoja kuzuia kutokea shambulio jingine kama hilo kwenye ardhi ya Marekani.

Familia za waathirika, maafisa wa polisi, wazima moto pamoja na wakuu wa mji wa New York, na makamu rais walikusanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Septemba 11, mahala ambako majengo mawili pacha ya World Trade Center yalibomolewa, na kusikiliza majina ya wale wote waliofariki yakisomwa

Watekaji nyara wa kundi la Al Qaeda waliteka ndege nne hapo Septemba 11 mwaka 2001, mbili zikigonga na kuangusha majengo ya World Trade Center, yatatu ikianguka kwenye jengo la Pentagon na ya nne kuanguka kwenye uwanja huko Pennsylvania.

Maadhimisho ya mwaka huu yanatokea mwaka mmoja baada ya Biden kumaliza vita vya Afghanistan vilivyoanzishwa miaka 20 iliyopita kwa

kuwaondoa wanejshi wa Marekani na kushuhudia kurudi madarakani kwa kundi la Taleban.

Lakini Biden hii leo ameahidi kwamba vita dhidi ya ugaidi vitaendelea. “Hatutapumzika. Hatutasahau. Hatutakubali kushindwa,” alisema Biden.

XS
SM
MD
LG