Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:21

Biden akashifu mpango wa bajeti ya Warepablikan


URais wa Marekani Joe Biden, akitoa hotuba yake kwenye chuo cha Prince George's Community College, Largo, Maryland. Sep 14, 2023.
URais wa Marekani Joe Biden, akitoa hotuba yake kwenye chuo cha Prince George's Community College, Largo, Maryland. Sep 14, 2023.

Wakati kukiwa na uwezekano wa kufungwa kwa shughuli za kifedha za serikali ya Marekani, Rais Joe Biden Alhamisi amekashifu mpango wa bajeti wa Repablikan, aliouita MAGAnomics, kwenye hotuba ambayo pia ilitetea mpango wa kiuchumi wa utawala wake.

“Kwa muda wote wanaotumia kunishambulia pamoja na mipango yangu, wenyewe hawasemi wanachotaka kufanya,” Biden alisema wakati akitoa hotuba kwenye chuo cha Prince George’s Community College, mjini Largo, jimbo la Maryland.

Amesema kwamba mpango wa Warepablikan umevuka mipaka kwa viwango ambavyo Marekani haijawahi kushuhudia.

Biden pia alikashifu mpango wa Repablikan wa kupunguza kodi kwa matajiri pamoja na makampuni makubwa, pamoja na kupunguza fedha kwenye program kama za malipo ya uzeeni na bima za afya za Madicare na Medicaid.

Aliongeza kusema kwamba mamilioni ya Wamarekani huenda wakapoteza bima zao za afya chini ya mpango wa kifedha wa wa-Repablikan.

Forum

XS
SM
MD
LG