Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:38

Trump adaiwa kufanya udanganyifu wa kibiashara kwa miaka mingi


Jaji mmoja amehukumu Jumanne kwamba, rais mstaafu wa Marekani, Donald Trump, alifanya udanganyifu kwa miaka mingi wakati anajenga himaya yake ya biashara ya majumba ambayo ilimpatia umaarufu mpaka kufika White House.

Jaji Arthur Engoron, alihukumu katika keshi iliyowasilishwa na mwanasheria mkuu wa New York, kwa kumkuta na mashitaka rais wa zamani wa Marekani na kampuni yake ya kudanganya mabenki, kampuni za bima, na nyingine kuhusu mali zake na kuongeza kiwango cha utajiri wake kwenye taarifa zilizotumika kuingia mikataba na kujipatia mikopo.

Jaji Engoron, alitoa amri kwa baadhi ya biashara za rais Trump kuwekewa vikwazo katika leseni zake ikiwa ni adhabu, na kuifanya isiwe na uwezo wa kufanya biashara New York, na kusema ataendelea kufanya uangalizi kuangazia namna taasisi ya Trump inavyofanya kazi.

Forum

XS
SM
MD
LG