Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 03:13

Seneta Coons apongeza azimio la kulaani rekodi mbovu ya haki za binadamu Eswatini


Mfalme Mswati III wa Eswatini
Mfalme Mswati III wa Eswatini

Seneta wa Marekani Chris Coons  alipongeza Baraza la Seneti kwa kupitisha kwa kauli moja azimio lake ambalo linalaani rekodi ya haki za binadamu ya serikali ya Eswatini na mauaji ya mwanaharakati wa haki za binadamu wa Eswatini Thulani Maseko.

Azimio hilo limewasilishwa na maseneta wengine wa Marekani Jim Risch, Mrepublikan kutoka Idaho, Cory Booker, Mdemokrat kutoka -N.J. na Tim Scott (Mrepublikan kutoka South Carolina) Sunday Shomari anaisoma taarifa kamili.

Eswatini ni ufalme kamili, wa mwisho, barani Afrika, chini ya utawala wa Mfalme Mswati III. Ukiukaji wa haki za binadamu katika ufalme huo ni jambo la kawaida, ikiwa ni pamoja na mauaji kinyume cha sheria, kuwekwa kizuizini kiholela, na vikwazo vikali vya uhuru wa kujieleza. Azimio hili linaitaka serikali ya Eswatini kufanya uchunguzi wa uwazi na wa kina kuhusu mauaji ya Maseko, wakili mashuhuri wa haki za binadamu huko Eswatini ambaye alipigwa risasi na kuuawa na mtu asiyejulikana Januari 21, 2023. Mamlaka ya Eswatini imeshindwa kutangaza mhatua zilizopigwa juu ya uchunguzi huru kuhusu mauaji ya Maseko, na mengi zaidi ni lazima yafanywe kuwawajibisha waliohusika na kulinda haki za binadamu nchini Eswatini.

Seneta Coons alisema anapongeza kupitishwa kwa azimio lake la pande mbili la kulaani rekodi ya haki za binadamu ya serikali ya Eswatini na mauaji ya kikatili ya Thulani Maseko, ambaye alikuwa mtetezi mkubwa wa haki za binadamu. Maseko alipigana bila kuchoka kuboresha haki za binadamu na uhuru wa raia katika ufalme huo. Hata hivyo, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kifo chake, hakuna mafanikio makubwa katika uchunguzi huru kuhusu mauaji yake ambayo yamepatikana. Kibaya zaidi, wanafamilia wake akiwemo mjane wake, Tanele Maseko wanaendelea kukabiliwa na unyanyasaji kutoka kwenye serikali.

Seneta Coons ni Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya masuala ya uendeshaji wa nchi na mambo ya nje (SFOPS), pia mwanachama wa Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya nje na Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Seneti la Haki za Kibinadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG