Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:03

Maseneta wa Marekani wawasilisha mswada wa kuongezewa muda kwa AGOA


PICHA YA MAKTABA: Seneta Chris Coons (Kulia) aliyesema ni kipaumbele cha juu kuidhinisha upya Sheria ya Ukuaji na Fursa kwa Afrika (AGOA) mwaka huu.
PICHA YA MAKTABA: Seneta Chris Coons (Kulia) aliyesema ni kipaumbele cha juu kuidhinisha upya Sheria ya Ukuaji na Fursa kwa Afrika (AGOA) mwaka huu.

Kundi la maseneta wa mirengo yote miwili ya kisiasa ya Marekani, limewasilisha mswada wa kutaka kuendeleza mkataba wa kibiashara kati ya Marekani na nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, kabla ya kumalizika muda wake mwaka ujao, msaidizi wa mmoja wa maseneta alisema Alhamisi.

Mswada huo uliwasilishwa na Maseneta Chris Coons, Mdemoktrat, na James Risch, Mrepublican wa hadhi ya juu katika Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Seneti. Maseneta wengine, Dick Durbin, Michael Bennet, Chris van Hollen, Todd Young na Mike Rounds - wanafadhili mswada huo kwa pamoja.

Msaidizi wa Coons alisema ni kipaumbele cha juu kuidhinisha upya Sheria ya Ukuaji na Fursa kwa Afrika (AGOA) mwaka huu.

Mswada huo, ambao ulionekana tu na shirika la habari la Reuters, unakusudiwa kuendeleza mpango huo wa AGOA kwa miaka 16, hadi mwaka 2041, na kusaidia nchi kutekeleza mikakati ya kunufaika nao.

Pi unanuiwa kudumisha manufaa kwa nchi kadiri zinavyozidi kuwa tajiri, na kuziwezesha kusalia katika mpango huo ikiwa zimedhamiria kuwa na mapato ya juu kwa miaka mitano badala ya kuziondoa iwapo zitafikia kikomo hicho kwa mwaka mmoja.

Chini ya mswada huo, nchi zitatathminiwa upya, ili kuamua kama zinastahiki kila baada ya mika miwili, badala ya kila mwaka kama ilivyo kwa sheria ya sasa. Lakini rais wa Marekani na baadhi ya viongozi wa bunge wanaweza kukagua ustahiki wa nchi, wakati wowote.

Forum

XS
SM
MD
LG