Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 08, 2024 Local time: 10:55

Russia yamhukumu Mmarekani kifungo cha muongo mmoja jela


Raia wa Marekani Robert Romanov Woodland akiwa mahakamani Julai 4, 2024. Picha na Reuters
Raia wa Marekani Robert Romanov Woodland akiwa mahakamani Julai 4, 2024. Picha na Reuters

Mahakama ya Russia siku ya Alhamisi imemhukumu raia wa Marekani Robert Romanov Woodland kifungo cha miaka 12 na nusu jela, baada ya kupatikana na hatia ya kutaka kuuza dawa za kulevya, mwanasheria wa Woodland na waendesha mashtaka wa Moscow wamesema.

Picha za video zilizotolewa na mamlaka zimemuonyesha Woodland akiwa ndani ya chumba cha kioo mahakamani akisikiliza kwa makini., lakini akiwa na hisia kidogo wakati hukumu ikisomwa.

Ofisi ya waendesha mashitaka wa Moscow imesema katika taarifa kuwa Woodland alikuwa sehemu ya kundi kubwa la uhalifu, alisafirisha takribani gramu 50 za mephedrone, aina ya amphetamine, kutoka kituo cha kuchukulia kilichopo nje ya Moscow na kupeleka kwenye nyumba yake iliyopo katika jiji hilo.

Alikamatwa wakati alipokuwa akiziweka dawa hizo katika eneo salama la maficho.

Woodland mwenye umri wa miaka 32 ni mmoja wa Wamerekani wanaoshikiliwa nchini Russia huku mahusiano ya mataifa hayo mawili yakiwa yameingia dosari kwa miongo kadhaa.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Moscow hakuweza kutoa maoni haraka.

Forum

XS
SM
MD
LG