Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 05:15

Putin, Xi, Erdogan katika mkutano wa nchi za Ulaya na Asia


Rais wa Russia Vladimir Putin na Xi Jinping wa Russia wakati wa mkutano wa SCO
Rais wa Russia Vladimir Putin na Xi Jinping wa Russia wakati wa mkutano wa SCO

Rais wa Russia Vladimir Putin na mwenzake wa China Xi Jinping, watakutana leo jumatano katika mkutano wa usalama na ulinzi unaohusisha nchi za Ulaya na Asia.

Mkutano huo unachukuliwa na Moscow na Beijing kuwa muhimu sana katika kukabiliana na ushawishi wa Marekani na washirika wake.

Putin na mwenzake wa China, wamepanua ushirikiano wa Shanghai, ulioanzishwa na Russia, China na nchi zilizo katikati mwa Asia mwaka 2001, na kujumulisha India, Iran na Pakistan kama mkakati wa kukabiliana na ushawishi wa nchi za magharibi.

Putin atafanya mikutano na viongozi wenzake pembezoni mwa mkutano huo unaofanyika Kazakh, Astana.

Atakutana na Xi, Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na viongozi wa Azerbaijan, Mongolia na Pakistan.

Forum

XS
SM
MD
LG