Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 01, 2024 Local time: 13:37

Satelaiti ya Russia yavunjika angani


Satelaiti isiyofanyakazi ya Russia imevunjika zaidi ya vipande 100 ikiwa kwenye mzunguko wa dunia, na kuwalazimimsha wanaanga kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kuchukua tahadhari kwa takriban saa moja.

Mabaki ya setelaiti hiyo sasa imeongeza takataka zaidi ambazo zipo katika mzunguko wa dunia, Idara ya Anga za Juu ya Marekani imesema.

Hakuna maelezo ya haraka juu ya kilichosababisha kuvunjika kwa satelaiti ya uchunguzi wa Dunia ya RESURS-P1, ambayo Russia ilitangaza kuwa imekufa mwaka 2022.

Komandi ya anga za juu ya Marekani, ikifuatilia mabaki yake, imesema hakuna tishio la haraka kwa satelaiti nyingine zilizo angani.

Tukio hilo limetokea Jumatano, komandi hiyo imesema. Ilitokea katika mzunguko wa dunia karibu na kituo cha anga za juu, na kuwafanya wanaanga wa Marekani kujificha katika sehemu maalumu kwa takriban saa moja, ofisi ya Kituo cha Anga cha Marekani, NASA imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG