Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 02:47

Makombora ya Russia yameua watu 4 Ukraine


Mabaki ya nyumba baada ya shambulizi Donetsk
Mabaki ya nyumba baada ya shambulizi Donetsk

Maafisa wa Ukraine wamesema leo Jumatano kwamba watu wanne wamefariki kutokana na mashambulizi ya kombora na ndege zisizokuwa na rubani za Russia.

Gavana wa wa mkoa wa Dnipro-petro-vsk, Serhiy Lysak, ameandika kwenye mtandao wa Telegram kwamba wanajeshi wa Russia wamewaua watu watatu na kujeruhi wengine 18.

Amesema kuna uharibifu umetokea na moto kuwaka kutokana na shambulizi hilo.

Mkoa wa kaskazini mashariki wa Kharkiv, maafisa wamesema kwamba shambulizi la Russia limeua mtu mmoja na kujeruhi wengine wanne.

Shambulizi pia limeharibu nyumba 10 na baadhi ya majengo ya biashara.

Jeshi la anga la Ukraine limesema kwamba shambulizi la Russia limehusisha makombora matatu aina ya Iskander-K na ndege zisizokuwa na rubani tano.

Jeshi limesema kwamba mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine umetungua makombora matano na ndege zote zisizokuwa na rubani.

Forum

XS
SM
MD
LG