Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:14

Ujasusi : Russia yaanzisha uchunguzi dhidi ya raia wa Marekani


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Russia imemkamata raia wa Marekani mjini Moscow ikimtuhumu kuwa jasusi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya nchi hiyo.

Maafisa wa Huduma ya Usalama wa Taifa ya Serikali Kuu ya Russia (FSB) wametoa tamko Jumatatu wakisema raia wa Marekani Paul Whelan amekamatwa Disemba 28 wakati akitekeleza vitendo vya ujasusi,”na kwamba wamefungua kesi ya uchunguzi wa makosa ya jinai dhidi yake.

Hata hivyo hawakutoa maelezo zaidi, lakini shirika la habari la serikali ya Russia TASS limesema kuwa Whelan anakabiliwa na kifungo iwapo atakutikana na makosa.

Hapakuwa na kauli iliyotolewa juu ya suala hilo na maafisa wa Serikali ya Marekani.

Kukamatwa huku kwa raia wa Marekani kumegongana na kashfa kadhaa za ujasusi ambazo zimeongeza mvutano kati ya Russia na nchi za Magharibi, ikiwemo kupewa sumu jasusi wa zamani aliyekuwa anatumikia pande mbili Sergei Skripal na binti yake huko Uingereza, pamoja na kuhukumiwa hivi karibuni raia wa Russia Maria Butina kwa vitendo vya ujasusi nchini Marekani kinyume cha sheria.

Habari za Whelan kukamatwa zimekuja chini ya masaa 24 baada ya Rais wa Russia Vladimir Putin kutuma salaam za mwaka mpya kwa Rais wa Marekani Donald Trump zinazo sema kuwa Moscow iko tayari kuendelea na mazungumzo na Washington juu ya mambo kadhaa.

Mnamo mwaka 2016, Izvestia, shirika la habari lenye mafungamano na Kremlin, limeripoti kuwa kulikuwa na raia wa Marekani 13 katika jela za Rashia wakati huo. Serikali ya Kremlin tangia wakati huo haijachapisha maelezo zaidi juu ya Wamarekani wengine walioko kizuizini nchini Russia.

​
XS
SM
MD
LG