Bozize, ambaye alichukua mamlaka nchini humo mwaka 2003 lakini alipinduliwa muongo mmoja baadaye, alihukumiwa bila kuwepo mahakamani siku ya Alhamisi, kulingana na hukumu iliyotumwa na wizara kwa shirika la habari la AFP.
Watoto wawili wa kiume wa rais huyo na washtakiwa wengine 20, ambao ni pamoja na viongozi wa waasi, pia walipewa hukumu hiyo bila kuwepo mahakamani.
Pia watuhumiwa hao walipatikana na hatia ya kuhatarisha usalama wa ndani na "mauaji", kulingana na hukumu ya mahakama ya rufaa katika mji mkuu wa Bangui.
Hukumu haikutoa maelezo zaidi kuhusiana na muda unaohusisha matendo hayo au uhalifu wenyewe.
Bozize, 76, ambaye alikuwa uhamishoni nchini Chad mpaka mwezi Machi alipohamia Guinea Bissau, anaongoza muungano wa makundi ya waasi yanayoitwa Coalition of Patriots for Change (CPC), yaliyoundwa Desemba 2020 kwa nia ya kumpindua mrithi wa Bozize, Faustin Archange Touadera.
Miongoni mwa waliohukumiwa mjini Bangui ni Ali Darassa, ambaye ni kiongozi wa kijeshi wa kundi kuu la wanamgambo ndani ya muungano huo wa CPC.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimeikumba Afrika ya Kati, mojawapo ya nchi maskini sana duniani, tangu muungano wa kundi la kiislamu lenye silaha linaloitwa Seleka ulipomuondoa Bozize madarakani mwaka 2013.
Bozize alianzisha wanamgambo wenye silaha wanaojulikana kama anti-Balaka, ambao wengi wao walikuwa Wakristo , ili kujaribu kurejea mamlaka.
Mzozo huo ulipungua nguvu kuanzia mwaka 2018, lakini nchi hiyo ilikuwa bado ikikabiliwa na machafuko na kuendelea kuwa ni maskini sana.
Ufaransa ambao ilikuwa utawala wa kikoloni, liliingilia kati kijeshi katika nchi hiyo isiyokuwa na utulivu mwaka 2013, ili kusaidia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vikiendelea kwa misingi ya madhehebu.
Desemba mwaka jana, Ufaransa iliwaondoa wanajeshi wake wa mwisho kutoka CAR huku uhasama ukiongezeka kwenye mitandao ya kijamii.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP
Forum