Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:46

Jeshi lamuweka kizuizini mtoto wa rais wa Gabon


Noureddin Bongo Valentin, mtoto mkubwa wa Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimb, akiwa Libreville Desemba 1, 2019. Picha na Picha na Steve Jordan / AFP.
Noureddin Bongo Valentin, mtoto mkubwa wa Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimb, akiwa Libreville Desemba 1, 2019. Picha na Picha na Steve Jordan / AFP.

Mtoto wa Ali Bongo Ondimba na washirika kadhaa wa rais wa Gabon aliyeondolewa madarakani, wameshtakiwa kwa tuhuma za rushwa na kuwekwa chini ya ulinzi, mwendesha mashtaka wa serikali aliliambia shirika la habari la AFP Jumatano.

Mtoto mkubwa wa rais Bongo, Noureddin Bongo Valentin na msemaji wa zamani wa rais Jessye Ella Ekogha, pamoja na watu wengine wanne walio karibu na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani, "wameshtakiwa na kuwekwa kizuizini kwa muda" alisema mwendesha mashtaka wa Libreville, Andre-Patrick Roponat siku ya Jumanne.

Rais Bongo mwenye umri wa miaka 64, ambaye alitawala taifa hilo la Afrika ya Kati, lenye utajiri wa mafuta tangu mwaka 2009, alipinduliwa na viongozi wa kijeshi Agosti 30, muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais.

Matokeo ya uchaguzi huo yalitajwa na upinzani na viongozi wa mapinduzi ya kijeshi kuwa ni ya udanganyifu, na pia kuutuhumu utawala wake umejaa ufisadi na utawala mbaya.

Siku yalipotokea mapinduzi, wanajeshi walimkamata mmoja wa watoto wa kiume wa rais Bongo na maafisa watano waandamizi wa baraza la mawaziri.

Televisheni ya taifa ilionyesha picha za watu waliokamatwa mbele ya masanduku yaliyojazwa pesa zinazodaiwa zilikutwa katika nyumba zao.

Baada ya mapinduzi, mke wa rais Bongo Sylvia Bongo Valentin aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika mji mkuu wa Libreville "kwa ajili ya usalama wake", kulingana na mamlaka.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG