Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:20

Raia wa Gabon washerehekea kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa


Wakazi wa Gabon wakisherehekea mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibunu mjini Libreville. Aug. 30, 2023.
Wakazi wa Gabon wakisherehekea mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibunu mjini Libreville. Aug. 30, 2023.

Raia wa Gabon Jumatano wamesherehekea kuwachiliwa Jumanne kwa wafungwa kadhaa wa kisiasa ambao walikuwa jela kwa miaka mingi bila ya kushtakiwa, hatua iliyokuwa imechukuliwa na  rais aliyeondolewa madarakani Ali Bongo Ondimba.

Wakati huo huo kiongozi wa mapinduzi Brice Nguema pia aliukaribisha ujumbe wa kwanza wa kimataifa uliongozwa na rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadera ukiwa umetumwa na viongozi wa mataifa ya Afrika ya kati, kufanya mashauriano ya kurejesha utawala wa kiraia baada ya kusitishwa uanachama wa Gabon kwenye muungano wa kikanda.

Utawala wa kijeshi nchini Gabon umesema umewaachilia watu kadhaa ambao walikuwa wakishikiliwa bila ya kufunguliwa mashitaka na serikali ya rais aliyeondolewa madarakani Ali Bongo. Miongoni mwa walioachiliwa na Jean Remy Yama kiongozi wa muungano wa vyama vya wafanyakazi unaojulikana kama Coalition of Gabon State Workers Trade Unions, ambaye amekuwa jela tangu Februari mwaka jana.

Televisheni ya serikali ya Gabon ilionyesha picha za watu kadhaa wakiwemo wafuasi wa upinzani wakisherehekea kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa. Wakati wa kuapishwa kwake kama rais wa muda wa Gabon Jumatatu, kiongozi wa mapinduzi Brice Oligui Nguema aliahidi kuwapa msamaha watu aliotaja kuwa wafungwa wa kihisia. Hata hivyo hakutoa idadi kamili ya wafungwa wa aina hiyo, lakini upinzani wa Gabon unasema kwamba ni wengi.

Nguema pia aliahidi kufanikisha kuwarejesha raia wote wa Gabon wanaoishi uhamishoni katika mataifa ya nje.

Forum

XS
SM
MD
LG