Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 26, 2024 Local time: 01:21

Jeshi la Gabon limesema litafungua tena mipaka ya nchi hiyo

Jenerali Brice Oligui Nguema (Kulia) wakati alipopewa nishani na Waziri Mkuu wa Gabon Alain Claude Bilie Bie Nze (kushoto) huko Libreville, Agosti 16, 2023. Picha na AFP.
Jenerali Brice Oligui Nguema (Kulia) wakati alipopewa nishani na Waziri Mkuu wa Gabon Alain Claude Bilie Bie Nze (kushoto) huko Libreville, Agosti 16, 2023. Picha na AFP.

Msemaji wa utawala wa kijeshi wa Gabon alisema kwenye televisheni ya taifa kwamba wameamua mara moja kufungua tena mipaka ya nchi kavu, baharini na anga kuanzia Jumamosi hii.

Jeshi la Gabon lilisema Jumamosi kwamba litafungua tena mipaka ya nchi hiyo iliyofungwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani rais wa zamani Ali Bongo.

Msemaji wa utawala wa kijeshi wa Gabon alisema kwenye televisheni ya taifa kwamba wameamua mara moja kufungua tena mipaka ya nchi kavu, baharini na anga kuanzia Jumamosi hii.

Kundi la wanajeshi 12 wa Gabon walitangaza siku ya Jumatano kwamba mipaka ya nchi hiyo imefungwa hadi itakapotangazwa tena katika taarifa iliyotangazwa kwenye kituo cha televisheni cha Gabon 24.

Jenerali Brice Oligui Nguema, mkuu wa kikosi cha ulinzi maalum kiitwacho Republican Guard siku ya Jumatano aliwaongoza maafisa katika mapinduzi dhidi ya Rais Ali Bongo Ondimba mtoto wa familia iliyotawala kwa miaka 55.

Forum

XS
SM
MD
LG