Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 26, 2024 Local time: 01:19

Jenerali Nguema awaahidi wananchi katiba mpya


Jenerali Brice Oligui Nguema (kulia) akitoa salamu wakati alipoapishwa kuwa Rais wa mpito wa Gabon, huko Libreville Septemba 4, 2023. Picha na AFP.
Jenerali Brice Oligui Nguema (kulia) akitoa salamu wakati alipoapishwa kuwa Rais wa mpito wa Gabon, huko Libreville Septemba 4, 2023. Picha na AFP.

Kiongozi wa kijeshi wa Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema amesema siku ya Jumatatu kuwa raia wa nchi hiyo watapata fursa ya kuwa na katiba mpya kupitia kura za maoni, na pia kuwepo kwa adhabu na kanuni mpya za uchaguzi.

Nguema, kiongozi wa kundi la maafisa wa jeshi walionyakua madaraka mwezi Agosti, dakika 30 baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi katika uchaguzi ambao walisema haukuwa wa kuaminika, kiongozi huyo wa jeshi alitoa hotuba mara tu baada ya kuapishwa kuwa raisi wa mpito na majaji wa mahakama ya kikatiba.

Kiongozi huyo wa mapinduzi alishangiliwa na wafuasi wake siku ya Jumatatu katika sherehe zilizotangazwa kupitia televisheni, sherehe zilizobumiwa kuwaonyesha wanajeshi kama wakombozi wa jamii iliyokuwa imekandamizwa.

Akishangiliwa na maafisa wa jeshi na viongozi wakati alipokuwa akiwasili katika sherehe hizo, na mara tu baadaye aliapishwa.

Kituo cha Televisheni ya Taifa kilionyesha picha za umati wa watu waliokuwa wakimshangilia, wakati maafisa walikuwa ndani ya magari ya kijeshi wakifyatua risasi baharini wakisheherekea hafla hiyo.

Katika hotuba yake, Nguema pia alipendekeza mageuzi ikiwemo katiba mpya itakayopitishwa kwa kura ya maoni, kanuni mpya za uchaguzi na kuzipa kipaumbele benki za ndani na makampuni kwa ajili ya maendeleo ya uchumi. Pia amesema wanasiasa walio uhamishoni wanakaribishwa kurudi nchini na wafungwa wa kisiasa kuachiliwa.

Jenerali Brice Oligui Nguema alipokuwa akihutubia Septemba 4, 2023. Picha na AFP.
Jenerali Brice Oligui Nguema alipokuwa akihutubia Septemba 4, 2023. Picha na AFP.

Hotuba yake ilikatishwa mara kwa mara kwa shangwe, alielezea mapinduzi hayo, ambayo yalihitimisha miaka 56 ya familia ya Bongo madarakani katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta, kama wakati wa ukombozi wa taifa hilo na udhihirisho wa mapenzi ya Mungu.

“Wananchi wanapokandamizwa na viongozi wao...ni jeshi ambalo linawarudishia utu wao," alisema. "Watu wa Gabon, leo nyakati za furaha ambazo kwa mababu zetu zilikuwa ndoto hatimaye zimetimia."

Jenerali Nguema pia ameahidi kuitisha "uchaguzi huru, wa wazi na wa kuaminika" bila ya kutoa muda maalum wa kurejesha utawala wa kiraia.

Katika hotuba yake pia amesisitiza kuwa mapinduzi hayo yameiokoa Gabon kutokana na umwagaji damu baada ya uchaguzi ambao ulikuwa "wazi wakilaghai."

Maafisa kadhaa wa serikali ya Bongo, wakiwemo makamu wa rais na waziri mkuu, walihudhuria sherehe hizo. Bongo mwenyewe bado yuko katika kizuizi cha nyumbani. Alichaguliwa mwaka 2009, akichukua wadhifa huo kutoka kwa marehemu babake aliyeingia madarakani mwaka 1967. Wapinzani wanasema familia haikufanya juhudi za kutosha kuwanufaisha watu wa Gabon ambao millioni 2.3 kutokana na utajiri wa mafuta na madini

Baadhi ya taariga hizi zinatoka Shirika la habari la Reuters na AFP

Forum

XS
SM
MD
LG