Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:51

Marekani na Norway kuzindua mfuko wa kusaidia kupambana na njaa barani Afrika


Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Samantha Power.
Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Samantha Power.

Marekani na Norway zimeahidi jumla ya dola milioni 70 za kuzindua mfuko ulioripotiwa nchini Norway kwa mara ya kwanza, kusaidia wakulima na biashara za kilimo barani Afrika, msemaji wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) alisema.

Shirika hilo lilisema hali ya njaa imezidi kuwa mbaya katika nchi kadhaa za Afrika, ikichochewa na migogoro ya silaha na hali mbaya ya hewa ambayo wanasayansi wamehusisha na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokana na utegemezi wa mafuta ghafi.

Tangazo hilo lililotolewa na Mkuu wa USAID Samantha Power na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Beathe Tvinne-reim, pembeni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, linakuja wakati Russia na China zikishindana na Marekani na Ulaya, kutafuta ufuasi au uungwaji mkono wa nchi zinazoendelea.

Mfuko huo unalenga kufikia jumla ya dola milioni 200 kupitia michango ya ziada kutoka kwa wafadhili na una uwezo wa kunufaisha karibu watu milioni 7.5, msemaji huyo alisema.

USAID na Norway zitatoa dola milioni 35 kila mmoja. Mfuko huo una uwezo wa kusaidia biashara 500 za kilimo ndogo na za kati, wakulima wadogo milioni 1.5 na karibu ajira 60,000 za sekta binafsi, na pia unalenga kuchochea mamia ya mamilioni ya dola zaidi katika ufadhili wa kibiashara kwa kupunguza hatari ya kuwekeza, kwa mujibu wa USAID.

Forum

XS
SM
MD
LG