Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:05

Janga la njaa lasababisha vifo Tigray, Ethiopia


Mwanamume wa Kiethiopia akiwa amebeba gunia la ngano mabegani mwake na kuipeleka katika Shirika misaada la Tigray kwa ajili ya kusambazwa huko Agula, Mei 8, 2021.
Mwanamume wa Kiethiopia akiwa amebeba gunia la ngano mabegani mwake na kuipeleka katika Shirika misaada la Tigray kwa ajili ya kusambazwa huko Agula, Mei 8, 2021.

Jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia linashuhudia upungufu mkubwa wa chakula kwa karibu miaka miwili sasa. Lakini hali imekua mbaya zaidi tangu mashirika ya misaada ya dharura kusitisha kwa muda ugawaji wa chakula kutokana na tuhuma za utumiaji mbaya wa misaada ya chakula inayotolewa.

Mashirika ya misaada ya dharura yalisitisha mipango yao ya kupeleka chakula kwa watu wanaokabiliwa na nja katika jimbo la Tigray baada ya ripoti ya wakaguzi wa Umoja wa Maraifa kueleza kwamba chakula cha msaada kinapelekwa kwa wanajeshi na wala si watu walokusudiwa.

Gaym Gebreselassie daktari bingwa mjini Adigrat anasema, moja kati ya wagonjwa wake alifariki mwizi mmoja uliyopita kufuatia operesheni ya kawaida kutokana na kidonda kilichozidi kuwa mbaya kutokana na njaa.

Mpwa wake alisimulia tukio hilo la kuhuzunisha la jinsi alivyofariki mama huyo wa watoto watano mwenye umri wa miaka 45, ambaye alikosa chakula kwa siku nyingi na aliomba maji akiwa katika siku yake ya mwisho duniani akiwa hospitali.

Aliomba kunywa maji, misuli yake ilikuwa imedhoofika kutokana na njaa ya muda mrefu, huku udenda ukimteremka kwenye kidevu chake, alisema.

Alifariki siku nne baadaye – ni mwathirika wa jangwa la njaa lililotabiriwa kuwa kubwa sana baada ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani na idara ya Msaada wa Kimataifa ya Marekani USAID kusitisha msaada wa chakula kwa Ethiopia mwezi huu, kutokana na misaa hiyo kutoroshwa na kutowafikia walengwa.

Sababu hasa za kifo chake haziwezi kuthibitishwa na taasisi za kujitegemea kwa kuwa waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia Tigray.

Watoto wake – wa mwisho ana umri wa miaka mitano tu -- sasa ni mayatima, na wanategemea jamaa ambao wenyewe hawawezi kujikimu.

Mhadhiri wa chuo kikuu huko Adigrat, mji unaopakana na Eritrea, Hailu alisema yeye mwenyewe alikula mara mwisho -- kipande cha mkate na chai -- masaa 48 yaliyopita.

Yeye na mke wake mara nyingi huwali chakula, alisema, huwa wanawapa watoto wao wachanga kwanza.

Lakini bado haitoshi.

"Mwanangu wa kiume huwa analalamika njaa na kutaka kula sehemu ya chakula cha dada yake ambaye pia ni mdogo," kijana huyo wa miaka 40 alisema.

Chanzo cha habari za taarifa hii zinatoka shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG