Taarifa ya USAID inasema ingependelea kuona misaada hiyo ya chakula inaanza kutolewa tena kwa njia ya kuaminika na inayostahiki na kuwafikia walengwa.
Msemaji wa Idara hiyo ameeleza katika taarifa yake kwamba USAID imegundua kwa kushirikiana na serikali ya Ethiopia kuwa kuna kampeni iliyoenea na iliyoratibiwa ya msaada wa chakula kupelekwa sehemu nyingine na kutowafikia watu wa Ethiopia kama ilivyopangwa.
Taarifa hiyo haikusema nani yuko nyuma ya kampeni hiyo na msaada umepelekwa wapi.
Marekani ndio mtoaji mkubwa wa misaada nchini Ethiopia ambako zaidi ya watu milioni 20 wanahitaji chakula kutokana na ukame na vita vilivyomalizika hivi karibuni katika mkoa wa kaskazini wa Tigray.
Uwamuzi huu umetolewa baada ya tangazo la USAID na Program, ya Chakula ya Umoja wa Mataifa, WPF mwezi uliyopita kusitisha msaada wa chakula kwa Tigray baada ya mashirika hayo kugundua misaada hiyo kupelekwa na kuuzwa masokoni.
Idara hiyo ya Marekani imejadili suala hilo na serikali ya Ethiopia na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alilizungumzia suala hilo na naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje Demeke Mekonnen kando ya mkutano wa mawaziri nchini Saudi Arabia wiki hii.
Karibu watu milioni 32 nchini Ethiopia, Kenya na Somalia wanakabiliwa na hali mbaya ya ukame ambao haujawahi kutokea na mashirika ya misaada yameonya juu ya hali ya njaa kuongezeka ikiwa hakuna misaada utatolewa kusaidia huduma za dhaura katika maeneo yaliyoathiriwa.
Forum