Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 06:28

Rais Tinubu awasili Beijing kuhudhuria kongamano la ushirikiano wa China na Afrika


Rais wa Nigeria akiwasili Beijing Septemba 1, 2024. Picha na Photo by Greg Baker / POOL / AFP.
Rais wa Nigeria akiwasili Beijing Septemba 1, 2024. Picha na Photo by Greg Baker / POOL / AFP.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amewasili Beijing siku ya Jumapili kuhudhuria mkutano wa viongozi kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) 2024 utakaofanyika katika mji mkuu wa China kuanzia Septemba 4 hadi 6.

Hii ni ziara ya kwanza ya Tinubu kuitembelea China tangu aingie madarakani.

China na Nigeria zimepata mafanikio makubwa ya ushirikiano chini ya mpango wa ujenzi wa miundo mbinu na ndani ya FOCAC na mifumo mingine.

China hivi sasa ni mshirika mkubwa sasa wa kibiashara wa Nigeria.

Nigeria pia ni moja ya nchi za kiafrika zenye idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma China. Tangu kuanzishishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili miaka 53 iliyopita, uaminifu wa kisiasa wa pande zote unaendelea kuimarika, na ushirikiano wa vitendo unaendelea kuzaa matunda, na kuwaweka mstari wa mbele katika ushirikiano wa China na Afrika.

Viongozi wengi wa Kiafrika, akiwemo mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, atawaongoza wajumbe katika mkutano huo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atahudhuria mkuatno huo kama mgeni maalum na mashirika husika ya kimataifa na ya kikanda pia yatahudhuria kama watazamaji.

Rais wa China Xi Jinping atatoa hotuba katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huo Septemba 5.

Forum

XS
SM
MD
LG