Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:00

Waandishi wasimulia mwamko wa matumizi ya teknolojia katika habari walioupata Beijing


Mwanahabari mkongwe wa Kenya Zubeidah Kananu
Mwanahabari mkongwe wa Kenya Zubeidah Kananu

Beijing inapeleka waandishi wa habari katika miji ya China kwenye maonyesho ya kitamaduni, teknolojia na utalii. Kinachokosekana, wanasema wachambuzi, ni picha isiyodhibitiwa ya China na ukiukaji wake wa haki za binadamu.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, mwanahabari mkongwe wa Kenya Zubeidah Kananu bado anakumbuka ziara ya mwezi Julai ambayo ilibadili mtazamo wake wa dunia.

“Mara tu unapofika huko, unahisi uko nyumbani mbali na nyumbani,” alisema Kananu.

Kananu, ambaye ni mhariri na rais wa chama cha wahariri wa Kenya, anasema alikuwa miongoni mwa wanahabari watano wakuu katika ziara ya vyombo vya habari iliyofadhiliwa na ubalozi wa China. Aliiambia Sauti ya Amerika kuwa “Ilitupa fursa ya kuona jinsi vyombo vya habari vilivyoendelea nchini China, teknolojia mpya wanazotumia, matumizi ya akili mnemba, matumizi ya ChatGPT katika kusimulia hadithi zao kila siku.”

Aliandika makala kuhusu Mao Zedong, mwanzilishi wa siasa za Kikomunisti nchini China. Makala yake ilichapishwa katika gazeti la Kenya, ni moja ya hadithi nyingi kuhusu China ambazo zipo katika ripoti zake nyingi.

Ziara hiyo ilimpa uzoefu wa kwanza wa kutangamana na watu wa China.

Watu wakitembea katika mitaa ya Dazhalan huko Beijing
Watu wakitembea katika mitaa ya Dazhalan huko Beijing

“Wanaithamini Afrika kwa njia ambayo sijawahi kushuhudia, wanakujulisha utamaduni wao kupitia chakula,” alisema.

China inaziona ziara hizo kama njia muhimu ya kubadilishana utamaduni, msemaji wa ubalozi wa China Liu Pengyu ameiambia VOA.

Anasema “Ushirikiano wa vyombo vya habari hauwezi tu kuboresha kiwango cha vyombo vya habari wenyewe, lakini pia kusaidia kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na ubalishanaji wa kitamaduni kati ya nchi.”

Juhudi za China ni pamoja na kufadhili ziara za vyombo vya habari huko China, hata kupeleka baadhi ya waandishi wa habari katika jimbo la Xinjiang ambako vyombo vya habari vya nchi za Magharibi zimeishtumu Beijing kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Mfanyakazi wa Taasisi ya Haki za Binaadamu Joyce Ho naye alisema kuwa “China kihalisi inataka, kwa ujanja mkubwa, kuwachukua maafisa hawa na kuwapeleka waandishi hawa wa habari wa kigeni mahali ambapo ukatilii huu wa kibinadamu unafanyika na kimsingi,”

“katika mazingira haya yaliyodhibitiwa na polisi, kuwambia watizame kote, hakuna tatizo lolote linaloonekana hapa,” aliongeza.

China imejaribu kuboresha taswira yake nje ya nchi kwa kuendeleza mtandao wa kimataifa wa vyombo vya habari na kusaini makubaliano na vyombo vya ndani kutoka Ulaya, Amerika Kusini na Afrika, kulingana na shirikisho la kimataifa la wanahabari.

Waandishi wa habari wakiwa Hangzhou
Waandishi wa habari wakiwa Hangzhou

Nchini Kenya, Beijing imeanzisha vyombo vya habari ambavyo vinaajiri mamia ya waandishi wa habari wa ndani.

Watangazaji wa China wanalenga kushindana na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vyenye maudhui katika lugha za nyumbani, ikiwemo Kiswahili.

Noah Midamba ni muhadhiri wa masomo ya sera za kigeni katika chuo kikuu cha Kenya cha KCA, amesema

“Wanataka kufanya kitu tofauti. Wanataka chochote wanachowekeza kihusishwe na taarifa nyingi na zipenye hadi kwenye ngazi ya kijiji.”

Wakati miradi mikubwa ya miundombinu inayofadhiliwa na China imekuwa mfano hai wa ushawishi wa Beijing barani Afrika, kuwakaribisha waandishi wa habari kutoka pembe zote za dunia, wanasema wataalam, ni mbinu yenye ufanisi.

Forum

XS
SM
MD
LG