Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:06

Mfalme wa Morocco awasamehe wanahabari watatu walioshtakiwa kwa ujasusi


Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita
Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita

Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita Jumatatu aliwasamehe wanahabari watatu ambao walikuwa wameshtakiwa kwa uhalifu wa kingono na ujasusi katika mashtaka yaliyolaaniwa sana na watetezi wa uhuru wa vyombo vya habari kama kulipiza kisasi dhidi ya ripoti za ukosoaji.

Omar Radi, Taoufik Bouachrine na Soulaimane Raissouni ni miongoni mwa watu 2,278 waliosamehewa wiki hii, kulingana na wizara ya sheria ya Morocco.

Msamaha huo ulitangazwa wakati Morocco ikiadhimisha kumbukumbu ya siku Mohammed wa Sita alipokabidhiwa Ufalme.

Kwa zaidi ya miaka minne, wanahabari hao walisimama imara dhidi ya juhudi kali za Morocco kuzima ukosoaji kutoka kwa vyombo vya habari na wanaharakati wa haki za binadamu.

Watetezi wa haki za kiraia, Bunge la Ulaya na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani katika taaarifa mbalimbali walilaani mashtaka hayo wakisema yamechochewa kisiasa.

Wanahabari hao watatu walikuwa wanajulikana kwa ripoti zao za ukosoaji na matamshi kuhusu serikali ya Ufalme na sera zake.

Forum

XS
SM
MD
LG