Katika wiki za hivi karibuni, Mamlaka inayodhibiti mawasiliano ya serikali ya Taliban, au ATRA, ilisimamisha leseni 17 za utangazaji zilizopewa vyombo vya habari katika jimbo la mashariki la Nangarhar.
Kituo cha radio cha kibinafsi cha Kawoon Ghag katika jimbo la Laghman pia kimefungwa, kulingana na mashirika yanayofuatilia uhuru wa vyombo vya habari.
“Miaka mitatu baada ya Kabul kutekwa, Taliban wanaendelea kuwakandamiza wanahabari na vyombo vya habari vinavyoendelea kufanya kazi nchini Afghanistan,” Beh Lih Yi, mtaratibu wa program katika shirika la Committee to protect Journalists kanda ya Asia, aliiambia VOA.
Alisema kupitia barua pepe kwamba“Mwezi Julai pekee, waandishi wa habari wawili, Sayed Rahim Saeedi na Mohammad Ibrahim Mohtaj, walikamatwa na maafisa wa ujasusi wa Taliban na polisi wa maadili.
Forum