Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:44

Viongozi wa Afrika wanaelekea China wakitafuta ufadhili wa miundombinu


Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Afrika nchini China.
Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Afrika nchini China.

China imeongeza uhusiano wake na mataifa ya Afrika katika muongo mmoja uliopita na kuwapatia mikopo ya mabilioni

Viongozi wa Afrika wanaelekea katika mji mkuu wa China wiki hii, wakitafuta ufadhili kwa ajili ya miradi mikubwa ya miundombinu wakati wakishuhudia ushindani mkubwa wa nguvu juu ya rasilimali na ushawishi katika bara hilo.

China imeongeza uhusiano wake na mataifa ya Afrika katika muongo mmoja uliopita, na kuwapatia mikopo ya mabilioni ambayo imesaidia kujenga miundombinu, lakini pia wakati mwingine ilizua utata kwa kuzitumbukiza nchi katika madeni makubwa.

China imepeleka maelfu ya wafanyakazi barani Afrika kujenga miradi yake mikubwa, wakati ikijiimarisha kwa rasilimali kubwa za bara hilo, ikiwemo shaba, dhahabu, Lithium na madini mengine adimu ya ardhini.

Beijing imesema mkutano wa wiki hii kati ya China na Afrika utakuwa tukio kubwa zaidi la kidiplomasia tangu janga la COVID-19, huku viongozi wa Afrika Kusini, Nigeria, Kenya na mataifa mengine yakithibitishwa kuhudhuria na wajumbe kadhaa wanatarajiwa kuwepo huko.

Forum

XS
SM
MD
LG