Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:53

Mataifa 52 ya Afrika yasaini hati ya maelewano na China ya ujenzi wa miundo mbinu


Rais wa China aliwa na viongozi wa nchi za baadhi ya nchi za Afrika katika kutano wa BRICS Agost 24, 2023. Picha na REUTERS/Alet Pretorius
Rais wa China aliwa na viongozi wa nchi za baadhi ya nchi za Afrika katika kutano wa BRICS Agost 24, 2023. Picha na REUTERS/Alet Pretorius

Mataifa 52 ya Afrika na Umoja wa Afrika yamesaini hati ya maelewano na China kuhusiana na ushirikaino wa Ujenzi wa Miundombinu (BRI).

China siku ya Alhamisi ilichapisha kitabu maalum chenye ripoti kuhusu matokeo ya ushirikiano wa China na Afrika ndani ya muundo wa juhudi za ujenzi wa miundo mbinu (BRI).

Ripoti hiyo imesema China na Afrika zimeinua uhusiano wao wa miundombinu kufikia hatua mpya.

Ikibainisha kuwa makampuni ya Kichina yanajihusisha na ujenzi na kufanya mabadiliko katika zaidi ya kilometa 10,000 za reli, takriban kilometa 100,000 za barabara kuu, madaraja yanayokadiriwa kuwa 1,000.

Aidha ripori hiyo imesema makampuni ya kichina yamejihusisha na ujenzi wa bandari 100, kilometa 66,000 za njia za kusambaza umeme na kilometas 150,000 za mitandao ya mawasiliano barani Afrika

Forum

XS
SM
MD
LG