Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:47

Russia yasema itatoa misaada ya kijeshi kuzisaidia nchi za Afrika


Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov akipiana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Yassine Fall huko Moscow Agosti 29, 2024. Picha na AP
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov akipiana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Yassine Fall huko Moscow Agosti 29, 2024. Picha na AP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesema wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal siku ya Alhamis kuwa nchi yake itatoa misaada ya kijeshi kuzisaidia nchi za Afrika.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Senegal Yassine Fall.

Aliongeza kuwa “Tuanasimamia hali ya eneo la Sahara na Sahel kuwa suala la makubaliano ya nchi za Afrika zenyewe.”

Misaada itakuwa zaidi kuimarisha ulinzi na kuboresha “kujiandaa kukabiliana na ugaidi wa vikosi vya kijeshi na huduma maalumu,” kulingana na Lavrov.

Pia amedai kuwa mazungumzo muhimu ya amani kati ya Russia na Ukraine “hayana umuhimu” baada ya Ukraine kuingia katika mkoa wa Kursk”

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Russia alisema,

“Rais wa Russia (Vladimir) Putin alikuja na mpango mwingine wa amani mwezi June, baada ya mipango yote ya amani iliyopita kuharibiwa na kuhujumiwa na utawala wa Kyiv na walezi wake wa Magharibi.”

“Kujitayarisha kwetu kwa mazungumzo kusingesababisha tatizo lolote na yoyote, ingawa, bila shaka, mazungumzo yeyote kuhusiana na suala hili yamekuwa hayana maana baada (ya Ukraine) kuingia katika mkoa wa Kursk, aliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG