"Ziara hizi ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano wa kihistoria, na ujirani mwema, urafiki na undugu, mshikamano na ushirikiano wa pande zote," ilisema taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Jumatano.
Tangu kuapishwa kwake mwanzoni mwa Aprili, Faye tayari amefanya ziara nyingi Afrika Magharibi, kwa majirani zake kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ivory Coast na Nigeria.
Safari yake siku ya Alhamisi itakuwa ya kwanza katika AES, muungano unaojumuisha Mali, Burkina Faso na Niger, nchi tatu zinazotawaliwa kijeshi, zilizoingia madarakani kupitia mapinduzi.
Mnamo Januari, nchi hizi tatu zilizoipa kisogo Ufaransa, zilitangaza kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo wanaishutumu haswa kwa kutii Paris na kutowaunga mkono vya kutosha katika vita dhidi ya wanajihadi.
Forum