Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:32

Senegal ina serikali mpya yenye mawaziri 25


Ousmane Sonko akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu na Rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, mjini Dakar, Senegal Aprili 2, 2024. REUTERS.
Ousmane Sonko akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu na Rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, mjini Dakar, Senegal Aprili 2, 2024. REUTERS.

Senegal ina serikali mpya yenye mawaziri 25 na mawaziri wadogo watano, Waziri Mkuu Ousmane Sonko alisema Ijumaa, kufuatia ushindi wa kishindo wa rais mwezi Machi.

Baraza hilo la mawaziri liliidhinishwa na Rais Bassirou Diomaye Faye, mwenye umri wa miaka 44, ambaye aliapishwa Jumanne na kumteua Sonko, mshirika wake wa karibu kuwa waziri mkuu. Faye alimrithi Rais Macky Sall, ambaye urais wake wa miaka 12 ulishuhudia kuongezeka kwa wimbi la kutoridhika kwa umma.

Baraza la mawaziri litaangaliwa kwa karibu baada ya Faye kutoa ahadi kali za kampeni kama vile kufuta sarafu ya CFA franc ya Afrika Magharibi. Amerudisha nyuma kidogo katika ahadi hiyo, lakini wiki hii mkaguzi huyo wa zamani wa kodi alito ahadi ukaguzi wa sekta ya mafuta, gesi na madini.

Uteuzi muhimu ni pamoja na Cheikh Diba kama waziri wa fedha. Diba hapo awali alikuwa mkurugenzi wa programu ya bajeti katika wizara ya fedha. Abdourahmane Sarr aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi.

Forum

XS
SM
MD
LG