Jeshi la Senegal lilisema Jumamosi kwamba liliizuia mashua iliyokuwa imebeba zaidi ya wahamiaji 200 wakijaribu kufika Ulaya, baada ya karibu watu 90 kufariki walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Atlantiki mapema mwezi huu.
Boti ilizuiliwa na boti ya doria katika eneo la uvuvi karibu na Lompoul kaskazini magharibi mwa Senegal siku ya Ijumaa ilikuwa imebeba watu 202, wakiwemo wanawake watano na mtoto mdogo, jeshi liliandika kwenye mtandao wa X.
Mapema mwezi Julai, mashua moja iliyokuwa imebeba takriban watu 170 waliotoka Senegal ilipinduka katika ufukwe wa Mauritania na kuuwa karibu watu 90.
Maafa hayo yalimfanya Rais wa Senegal Ousmane Sonko kuwataka watu kutohatarisha maisha katika safari za Bahari ya Atlantiki kwenye boti zilizojaa kupita kiasi ambazo mara nyingi hazina uwezo wa kusafiri baharini.
Lakini njia hiyo inazidi kutumiwa huku mamlaka zikifanya ufuatiliaji zaidi katika Bahari ya Mediteranian.
Forum