Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:06

Rais wa Senegal ametoa wito wa mazungumzo ya amani Mali na Niger


Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye.
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye.

Viongozi wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso walijiondoa kutoka ECOWAS mapema mwaka huu

Rais wa Senegal na mpatanishi wa ECOWAS, Bassirou Diomaye Faye ametoa wito leo Jumatatu kwa mazungumzo na maridhiano ya amani na nchi tatu ambazo hivi karibuni zilijiondoa na jumuiya hiyo.

Viongozi wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso walijiondoa kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi mapema mwaka huu na kuunda shirikisho lao siku ya Jumamosi.

Ramani ya Mali na nchi zilizo jirani nae.
Ramani ya Mali na nchi zilizo jirani nae.

Viongozi wa ECOWAS walikutana mjini Abuja Jumapili na kulaani “ukosefu wa maendeleo katika ushirikiano” na mamlaka za Burkina Faso, Mali na Niger, ambao waliingia madarakani katika mfululizo wa mapinduzi ya hivi karibuni.

“Hatuwezi kusimama bila mwelekeo,” Rais Faye wa Senegal alisema katika video iliyobandikwa Jumatatu. “Jukumu letu ni kufanya kazi ya kumleta kila mtu karibu na maridhiano, kuhakikisha kuna nafasi ya mazungumzo,” alisema huku akiapa kwamba umoja huo utafanya kazi kuelekea uletaji amani.

Forum

XS
SM
MD
LG