Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 12:47

Rais Ramaphosa apata COVID-19 na kuanza karantini


Rais wa Afrika Kusini aambukizwa COVID-19
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:36 0:00

Rais wa Afrika Kusini aambukizwa COVID-19

Rais Cyril Ramaphosa alianza kujisikia vibaya baada ya kuondoka kwenye sala ya kumbukumbu ya kitaifa ya kutoa heshima kwa Naibu Rais wa zamani FW de Klerk mjini Cape Town mapema jana Jumapili taarifa hiyo kutoka ofisi ya rais iliongeza

Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa mwenye umri wa miaka 69 alipimwa na kugundulika ana COVID-19 siku ya Jumapili ingawa anaonyesha dalili ndogo tu za ugonjwa huo ofisi ya rais ilisema.

Rais alianza kujisikia vibaya baada ya kuondoka kwenye sala ya kumbukumbu ya kitaifa ya kutoa heshima kwa Naibu Rais wa zamani FW de Klerk mjini Cape Town mapema jana Jumapili taarifa hiyo iliongeza.

Katika sala ya kumbukumbu Ramaphosa akiwa amevaa barakoa alizungumza kwa heshima kwa kiongozi wa mwisho wa serikali ya wazungu wachache nchini Afrika kusini ambaye alisaidia kumaliza ubaguzi wa rangi.

Rais Ramaphosa ambaye amepata chanjo kamili ya COVID-19 amejiweka katika karantini hivi sasa huko Cape Town na amekabidhi majukumu yote kwa Naibu Rais, David Mabuza ofisi ya raia iliongeza.

XS
SM
MD
LG