Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:58

Afrika kusini yatoa heshima za mwisho kwa De Klerk


F.W. de Klerk, Rais wa mwisho utawala wa wazungu Afrika kusini
F.W. de Klerk, Rais wa mwisho utawala wa wazungu Afrika kusini

De Klerk alifariki Novemba 11 akiwa na miaka 85 kufuatia maradhi ya saratani. Alihudumu kama Rais mwaka 1989-1994 na anakumbukwa kwa kuiongoza  Afrika kusini katika kipindi cha mpito kutoka utawala wa wazungu wachache hadi uchaguzi wa kwanza usio wa kibaguzi 1994

Afrika kusini leo Jumapili ilitoa heshima rasmi kwa FW de Klerk, Rais wa mwisho wa utawala wa wazungu ambaye alimtoa gerezani Nelson Mandela na kuiongoza nchi kutoka kwa ubaguzi kuelekea kwenda kwenye demokrasia.

De Klerk alifariki Novemba 11 akiwa na umri wa miaka 85 kufuatia mapambano ya maradhi ya saratani. Siku nne za maombolezo ya kitaifa zilitangazwa kwa heshima yake. Alihudumu kama Rais kuanzia mwaka 1989 hadi 1994 na anakumbukwa zaidi kwa kuiongoza Afrika kusini katika kipindi cha mpito kutoka katika utawala wa wazungu wachache hadi uchaguzi wa kwanza usio wa kibaguzi mwaka 1994.

Pia De Klerk alishirikiana tuzo ya Amani ya Nobel na Mandela mwaka 1993 baada ya kumwachilia kutoka gerezani mwaka 1990. Mandela baadaye wakati huo alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini baada ya chama chake cha African National Congress kushinda uchaguzi wa mwaka 1994.

Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa

Rais Cyril Ramaphosa, alihudhuria misa leo asubuhi katika kanisa la kiprotestanti la Groote Kerk mjini Cape Town, moja ya makanisa zamani sana Afrika kusini, ili kutoa maelezo yake kwa heshima ya De Klerk.

XS
SM
MD
LG