Katika taarifa ya kwanza rasmi ya makampuni hayo ya kutengeza dawa kuhusu ufanisi wa chanjo yao dhidi ya Omicron, BioNTech na Pfizer zimesema dozi mbili hazikuonyesha ufanisi wa kutosha wa kudhibiti kirusi hicho, lakini dozi ya tatu imeongeza ufanisi wa kukabiliana na kirusi cha Omicron kwa asilimia 25.
Lakini kituo cha utafiti chenye makao yake Durban Afrika kusini, African Health Institute kinasema matokeo ya utafiti wake yameonyesha kwamba chanjo zilizopo dhidi ya corona, zina ufanisi mdogo wa kudhibiti kirusi cha Omicron.