Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:59

Afrika kusini kuanza kutoa Booster ya COVID-19 kwa wakaazi wake


Mkaazi wa Cape Town akipatiwa chanjo ya COVID-19 hapo Dec. 8, 2021.
Mkaazi wa Cape Town akipatiwa chanjo ya COVID-19 hapo Dec. 8, 2021.

Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya nchi hiyo kuripoti ongezeko kubwa kabisa la watu walioambukizwa kwa siku moja kutokana na virusi vya corona. Crisp alisema watu wa kwanza watakaopewa BOOSTER ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60

Mkurugenzi mkuu wa afya wa Afrika kusini Nicolas Crisp alisema leo Ijumaa kwamba nchi yake inajiandaa kutoa dozi ya nyongeza au BOOSTER ya chanjo ya COVID-19 ya Pfizer na Johnson & Johnson.

Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya nchi hiyo kuripoti ongezeko kubwa kabisa la watu walioambukizwa kwa siku moja kutokana na virusi vya corona. Crisp alisema watu wa kwanza watakaopewa BOOSTER ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60.

Aliongeza kusema kwamba chanjo hizo zitatolewa miezi sita baada ya kupata dozi ya pili kwa wale waliopata chanjo ya Pfizer ambapo kwa Johnson & Johnson inatolewa dozi moja pekee na hata hivyo hapo awali Johnson & Johnson ilitolewa kwa wafanyakazi wa afya pekee na kwamba hivi karibuni chanjo hiyo itapatikana kwa kila mtu.

XS
SM
MD
LG