Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:22

20,000 waambukizwa Corona, 36 wafariki Afrika kusini


Kijana mwenye umri wa miaka 16 Ziyaad Benjamin akipokea chanjo dhidi ya Corona mjini Cape Town, Afrika kusini. Ocktoba 20. 2021
Kijana mwenye umri wa miaka 16 Ziyaad Benjamin akipokea chanjo dhidi ya Corona mjini Cape Town, Afrika kusini. Ocktoba 20. 2021

Afrika kusini imeripoti kwamba karibu watu 20,000 wameambukizwa virusi vya Corona tangu aina mpya ya virusi hivyo, Omicron iliporipotiwa. Watu 36 wamefariki dunia.

Idadi hiyo ya maambukizi na vifo imetokea jumatano pekee.

Haijabainika wazi kuhusu idadi ya maambukizina vifo kutokana na Omicron, lakini wataalam wanasema kwamba aina mpya ya virusi hivyo inapelekea kutokea wimbi la nne la maambukizi.

Takwimu za taasisi ya kitaifa kuhusu magonjwa ya kuambukiza Afrika kusini zinasema kwamba watu milioni 3 wameambukizwa Corona na 90,000 wamefariki dunia nchini humo, tangu mlipuko wa Corona ulipotokea.

Utafiti wa awali umebaini kwamba virusi vya Omicron vinasambaa kwa kasi sana kuliko aina yoyote ile ya virusi vya Corona lakini sio hatari sana, huku wanaoambukizwa, haswa kwa waliopata chanjo, wakiripotiwa kupata nafuu bila kulazwa hospitalini.

Uchumi wa Afrika kusini umeathirika sana kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Nchi hiyo imewekewa vikwazo vya usafiri kimataifa kutokana na kugunduliwa kwa maambukizi ya Omicron.

XS
SM
MD
LG