Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amewaambia waandishi wa habari mjini New York Alhamisi kuwa Tehran itaruhusu kufanyika uchunguzi wa kina zaidi wa programu yake ya nyuklia iwapo tu Washington itaiondoshea vikwazo vya kiuchumi.
Lakini pendekezo hilo, ambalo Zarif amelielezea kama ni “hatua muhimu” alisema limepuuziwa.
Afisa wa ngazi ya juu wa uongozi wa Marekani amesema, “Rais amerejea kusema kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa Iran.
Washington inajaribu kuishinikiza Tehran kukubaliana na viwango finyu zaidi vya uwezo wake wa nyuklia, kuzuia programu yake ya makombora ya balistiki, na kuacha kusaidia wapiganaji wake walioko maeneo mengine katika ushindani wake na nchi za Ghuba ya Arabuni zinazosaidiwa na Marekani.