Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 12:02

Prince Harry hakufika mahakamani siku ya kwanza ya kesi yake dhidi ya wachapishaji wa gazeti la udaku la Uingereza


FILE - Britain's Prince Harry arrives in the gardens of Buckingham Palace in London, Jan 16, 2020.
FILE - Britain's Prince Harry arrives in the gardens of Buckingham Palace in London, Jan 16, 2020.

Kesi iliyokuwa inatarajiwa ya Mwanamfalme Harry dhidi ya wachapishaji wa gazeti la Daily Mirror imeanza kusikilizwa Jumatatu bila ya yeye kuwepo mahakamani – na jaji alikuwa hajafurahishwa.

Wakili wa Harry alisema mteja wake Duke wa Sussex hatokuwepo mahakamani kutoa ushahidi baada ya matamshi ya ufunguzi kwa sababu alipanda ndege kutoka Los Angeles baada ya kusherehekea sikukuu ya binti yake Lilibet, aliyetimiza umri miaka 2, siku ya Jumapili.

“Nimeshangazwa kidogo sikutarajia hilo.” Jaji Timothy Fancourt alisema, akieleza alikuwa ameagiza kuwa Harry afike mahakamani siku ya kwanza ya kesi yake.

Wakili wa kampuni ya Gazeti la Mirror, Andrew Green, alisema alikuwa “amekerwa sana” kwa kukosekana Harry katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa kesi.

Waandishi wa Habari wakiwa nje ya Mahakama Kuu wakimtarajia Prince Harry kuwasili, London, Juni 5, 2023.
Waandishi wa Habari wakiwa nje ya Mahakama Kuu wakimtarajia Prince Harry kuwasili, London, Juni 5, 2023.

Kesi dhidi ya kampuni nya Mirror Group ni ya kwanza kati ya kesi kadhaa zilizofunguliwa na mwanamfalme huyo dhidi ya vyombo vya habari zitakazofanyika baadae, na moja ya madai matatu dhidi ya wachapishaji ni kumchunguza kinyume cha sheria katika ushindani wao wa kupata habari za kipekee juu ya familia ya kifalme.

Wakili wa Harry, David Sherborne, alisema udukuzi wa simu na njia za ukusanyaji habari kinyume cha sheria zilifanyika kwa kiwango kikubwa, haiwezekani kwa mchapishaji wa magazeti kumtumia mchunguzi binafsi kutafuta dosari za mwanamfalme mara moja tu, kitu ambacho wamekiri kufanya.

“Kusudio hilo linahalalisha njia iliyotumiwa na mshtakiwa,” Sherborne alisema.

Habari kuhusu Harry zilikuwa zinauza magazeti kwa wingi, na takriban makala 2,500 ziliripoti kila upande wa maisha yake – kuanzia ugonjwa wake akiwa shuleni na mpaka kunyanyuka na kuanguka kwake akiwa na marafiki wa kike, Sherborne alisema.

“Hakuna wakati katika maisha yake ambapo alikuwa salama kutokana na harakati hizi za magazeti,” Sherborne alisema. “Hapakuwa na mipaka wala kuheshimu nafasi yake ya kifalme.

Kampuni ya Mirror Group imesema ilitumia nyaraka, matamko yaliyotolewa kwa umma na vyanzo vingine kuripoti kwa njia halali juu ya mwanamfalme.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG