Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:58

Prince Harry na Meghan wafuatiliwa na waandishi wapigapicha mjini New York


Prince Harry akiwa na mkewe Meghan, na mama wa Meghan, Doria Ragland. 20 Sept. 2018 (arquivo)
Prince Harry akiwa na mkewe Meghan, na mama wa Meghan, Doria Ragland. 20 Sept. 2018 (arquivo)

Tukio hilo lilitokea baada ya familia hiyo kuhudhuria sherehe za tuzo zilizofanyika mjini New York zilizoandaliwa na Ms.Foundation for Women ambapo Meghan alipatiwa tuzo kwa kazi zake anazofanya

Prince Harry wa Uingereza akiwa na mke wake Meghan pamoja na mama wa Meghan walijikuta wakifuatiliwa na gari lililowabeba waandishi wanaochukua picha, msemaji wa Harry amesema leo Jumatano.

Tukio hilo lilitokea baada ya familia hiyo kuhudhuria sherehe za tuzo zilizofanyika mjini New York zilizoandaliwa na Ms.Foundation for Women ambapo Meghan alipatiwa tuzo kwa kazi zake anazofanya.

Picha ambazo zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii zinawaonyesha Harry, Meghan na mama wa Meghan, Doria Ragland wakiwa ndani ya Taxi. "Jumanne usiku The Duke na Duchess wa Sussex na Miss Ragland walijikuta wakifuatiliwa na gari lililokuwa na wapigapicha", msemaji alisema katika taarifa hiyo.

Harry na Meghan walijiondoa katika jukumu la kazi za kifalme mwaka 2020 na walihamia Marekani kwa kile walichokielezea usumbufu wa hali ya juu wa vyombo vya habari.

Harry kwa muda mrefu amekuwa akizungumza kuhusu hasira zake za kufuatiliwa na vyombo vya habari ambapo anavilaumu kupelekea kifo cha mama yake Princess Diana ambaye alifariki wakati gari lake lilipopata ajali likiwa linawakimbia waandishi wa habari waliokuwa wakimfuatilia mjini Paris, Ufaransa.

XS
SM
MD
LG