Mfalme Charles III alitembea nyuma ya gari lililobeba jeneza la malkia. Akiungana na watoto wake William na Harry, na ndugu zake, Anne, Andrew na Edward.
Umati mkubwa wa watu unatarajiwa kuwepo katika barabara hiyo, huku maelfu ya watu wakitarajiwa kusafiri kwenda Westminster kutoa heshima zao.
Gwaride hilo litafanyika huku kukiwa na ufyatuaji wa bunduki kwenye eneo la Hyde Park na kupigwa kwa kengele ya Big Ben ya bungeni.
Mwili wa Malkia utalazwa kwa siku nne katika Ukumbi wa Westminster wa karne 11. Ukumbi huo utakuwa wazi kwa saa 23 kila siku kwa ajili ya wageni na utalindwa na wanajeshi kutoka nyumba ya kifalme.
Elizabeth alifariki Septemba 8 huko katika Makazi ya Balmoral katika eneo Scottish Highlands, sehemu ambayo Malkia aliipenda na ndipo Charles alipokuwa mfalme.
Mazishi ya malkia yamepangwa kufanyika Septemba 19 huko Westminster Abbey. Jeneza hilo baadae litachukuliwa kwenda Windsor kwa ajili ya ibada ya mazishi, ambapo mume wa malkia, Prince Philip, ndipo alipozikwa mwezi Aprili 2021.
Baadhi ya taarifa katika repoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, Reuters na AFP